Home Uncategorized BEKI WA TANZANIA PRISONS AWAKIMBIZA MABEKI WOTE BONGO KWA KUCHEKA NA NYAVU

BEKI WA TANZANIA PRISONS AWAKIMBIZA MABEKI WOTE BONGO KWA KUCHEKA NA NYAVU


SALUM Kimenya beki kiraka anayekipiga ndani ya Klabu ya Tanzania Prisons amewakimbiza mabeki wote wanaokipiga ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kucheka na nyavu.

Kabla ya ligi kusimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona, Kimenya alicheka na nyavu mara tano.

Idadi hiyo ya mabao ni kubwa kufungwa msimu huu kwa mabeki wote ndani ya Ligi Kuu Bara wanaokipiga kwenye timu zote za Bongo ikiwa ni pamoja na Simba, Yanga, Azam FC, Lipuli na Kagera Sugar.

Kwa Simba beki mwenye mabao mengi ni Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ mwenye mabao mawili huku kwa Azam FC Nicolas Wadada ametupia bao moja.

SOMA NA HII  AZAM FC AKILI ZIPO KWENYE UBINGWA