Home Uncategorized ARSENAL BADO INA MATUMAINI

ARSENAL BADO INA MATUMAINI


MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa licha ya kupokea kichapo cha mabao 3-0 mbele ya Manchester City ana imani kikosi chake kitarejea kwenye ubora wake.
City iliyo chini ya Pep Guardiola, iliwashushia Arsenal kichapo cha mabao matatu kupitia kwa Raheem Sterling dakika ya 45, Kevin De Bruyne aliyefunga kwa penalti dakika ya 51 na msumari wa tatu ulijazwa kimiani na Phil Foden dakika ya 90.
Beki wa Arsenal, David Luis alitolewa nje kwa kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 49 baada ya kumchezea faulo Riyad Mahrez anayekipiga ndani ya City jambo ambalo liliwafanya Arsenal wazidi kubanwa mbavu na wapinzani wao.
Matokeo hayo yanaifanya Manchester City izidi kujikita nafasi ya pili ikiwa na pointi zake  60 huku Arsenal ikiwa nafasi ya 9 na pointi zake kibindoni 40 zote zimecheza mechi 29 ndani ya Ligi Kuu England.
SOMA NA HII  BIASHARA UNITED V YANGA, NGOMA NI NZITO, CHEKI REKODI ZAO