Home Uncategorized PAMBA SC YAAHIDI KUENDELEA KUTOA SAPOTI ZAIDI KWENYE MICHEZO

PAMBA SC YAAHIDI KUENDELEA KUTOA SAPOTI ZAIDI KWENYE MICHEZO


UONGOZI wa Pamba SC umesema kuwa utaendelea kutoa sapoti kwenye Academy za nchini Tanzania kwa kuwa wanatambua malengo yao ni kukuza vipaji.

Akizungumza na Salehe Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Pamba, Aleem Albhai amesema kuwa wamekuwa wakinufaika na Academy kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwatumia wachezaji wao katika timu yao.

“Tumekuwa tukipata ushirikiano mzuri kutoka kwenye hizi Academy hasa kwa upande wa wachezaji, nina amini wachezaji wengi ambao wanaitumikia Pamba huwa wanatoka huko kwenye Academy na wanafanya kazi vizuri.

“Tutaendelea kutoa sapoti kwa kadri tutakavyoweza kwani malengo yetu ni kuona kwamba mpira unakua na vijana wanapata nafasi ya kufikia yale wanayofikiria zaidi,” amesema.

Hivi karibuni, Pamba ilitoa misaada ya mipira 30 kwa Academy za Mwanza, miongoni mwa Academy zilizopatiwa Mipira ni pamoja na Marsh Athletic Academy, Alliance Academy, Tsc Academy, Mandozi Academy, Mweita Academy.

SOMA NA HII  EXCLUSIVE: BARAKA MPENJA ATAJA TIMU ANAYOSHABIKIA - VIDEO