Home Uncategorized KIMENUKA TENA! MAPACHA WA P-SQUARE KUBURUZANA MAHAKAMANI

KIMENUKA TENA! MAPACHA WA P-SQUARE KUBURUZANA MAHAKAMANI


Wasanii maarufu nchini Nigeria, ambao ni mapacha Peter na Paul Okoye (P-Square) huenda wakaburuzana mahakamani kwa kile kinachodaiwa kuwa Paul ametumia picha ya mwenzake kwenye tangazo la tamasha lake nchini Angola.

Peter ambaye ni mlalamikaji, amesema kuwa anatarajia kwenda mahakamani kumshtaki ndugu yake, Paul kwa kutumia picha zake kwa ajili ya kutangaza tamasha hilo la muziki.

“Kwahiyo wameamua kutumia picha yangu ili wauze tiketi za show yao huko Angola. “Nyie mapromota na uongozi mzima, mwanasheria wangu atalifuatilia suala hilo mapema iwezekanavyo,” ameandika Peter kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo, tayari Paul Okoye ameshafanya shoo yake juzi Jumapili Mei 26, 2019, usiku nchini Angola.

Peter na Paul ni mapacha na zamani waliunda kundi la P-Square ambalo lilipata umaarufu zaidi duniani kupitia nyimbo kadha wa kadha ikiwemo Personally, Temptation na nyinginezo.

Kwa sasa kundi hilo limevunjika kwa sababu mbalimbali ikiwemo za maslahi binafasi na kifamilia, japo kumekuwa na masuluhisho kadhaa ya kurudisha kundi hilo.

SOMA NA HII  TFF, SIMBA WAJICHANGANYA KUHUSU SHOMARI KAPOMBE