Home Uncategorized SINGIDA UNITED BANA, YAITANGAZIA HATARI YANGA

SINGIDA UNITED BANA, YAITANGAZIA HATARI YANGA


UONGOZI wa Singida United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Ramadhan Nswanzurimo umesema kuwa hauna mashaka na mchezo wao wa kesho, Januari 22 dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa Namfua, Singida.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu ila wamejipanga kupata ushindi.

“Tunatambua Yanga ni timu bora na ina wachezaji wenye uzoefu ila hilo halitupi mashaka tupo tayari kuona namna gani tutashinda.

“Mashabiki wajitokeze kutupa sapoti kwani timu imekuwa ikipita kwenye wakati mgumu ila kwa sasa tumeanza kurejea kwenye ubora,” amesema.

Singida United ipo nafasi ya 16 ina pointi 10 imeshinda mechi mbili pekee katika mechi 16 ilizocheza mpaka sasa.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA APEWA ONYO KALI NA BODI YA LIGI, POLISI TANZANIA WAVURUMISHWA FAINI