Home Uncategorized MATOKEO MABAYA YAISIKITISHA YANGA, UJUMBE HUU WATUMWA SINGIDA

MATOKEO MABAYA YAISIKITISHA YANGA, UJUMBE HUU WATUMWA SINGIDA


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umesikitishwa na matokeo ya mechi zake mbili zilizopita na kuomba sapoti kwa mashabiki wao.

Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael lipoteza mechi mbili mfululizo kwa kuchapwa mabao 3-0 na Kagera Sugar kisha ikapoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Azam FC.

Ofisa uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa hawajafurahishwa a aina ya matokeo hayo mpaka sasa wanajipanga kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Singida United utakaochwezwa kesho, Namfua.

“Kwa matokeo ambayo tumeyapata tumesikitishwa na matokeo yaliyopita. Mashabiki wa Yanga wanapaswa kutokata tamaa, waendelee kuipa sapoti timu, sasa tunajipanga kumalizana na Singida United kwao,”  amesema Nugaz.

Yanga ipo nafasi ya nane kwenye msimamo ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 25 kibindoni.

SOMA NA HII  YANGA WAREJEA DAR, HESABU ZAO ZIPO KWENYE KOMBE TU