Home Uncategorized YANGA IPO KAMILI GADO KUIVAA PRISONS

YANGA IPO KAMILI GADO KUIVAA PRISONS

 


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara ambao utakuwa ni wa raundi ya pili dhidi ya Tanzania Prisons.


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Desemba 31, Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa.


Yanga inakutana na Prisons ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa.


Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na wanahitaji pointi tatu muhimu.

SOMA NA HII  AZAM FC YAFIKIRIA KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU BARA