Home Habar za Usajili Simba KUHUSIANA NA MAJERAHA YA FEI TOTO…ALL MAYAY AIBUKA NA HILI JIPYA..AMTAJA AUCHO….

KUHUSIANA NA MAJERAHA YA FEI TOTO…ALL MAYAY AIBUKA NA HILI JIPYA..AMTAJA AUCHO….


MASTAA wa zamani wa Yanga wamewashusha presha mashabiki kwa kusema hata kama Feisal Salum ‘Fei Toto’ hayupo kikosini bado kuna watu spesho kama Khalid Aucho, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Saido Ntibazonkiza wanaoweza kukiwasha bila wasiwasi wowote.

Wameweka wazi kukosekana kwa Fei Toto ambaye atakuwa nje kwa wiki mbili akisumbuliwa na goti hakuwezi kumpa presha kocha wa timu hiyo, Nasreddine Nabi anayeweza kuwatumia Aucho, Sure Boy, Saido na Zawadi Mauya kunaondoa pengo lake.

Yanga ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar, Sure Boy akicheza kwa kiwango cha juu, akikosekana Fei Toto aliyekuwa anauguza majeraha kabla ya juzi kuumia tena akiwa na na timu ya taifa ‘Taifa Stars’.

Ali Mayay ambaye alitamba na Yanga na Taifa Stars, alisema upana wa kikosi cha Yanga una wachezaji wasiopishana uwiano wa viwango, unaondoa presha pindi mchezaji mmoja anapokosekana, akitoa mfano wa Fei Toto. “Dhidi ya Kagera Sugar, Fei Toto alikosekana na Sure Boy alicheza kwa kiwango cha juu na Yanga ikishinda mabao 3-0, hakuna pengo lililonekana pia dhidi ya Mbeya City alianza Mauya na Fei Toto kaanzia benchi,” alisema Mayay na kuongeza;

“Nabi anaweza akatumia mfumo wa 4-3-3 ama 4-2-3-1, maana ana viungo wengi wanaoweza kulimudu vyema eneo hilo, kama Saido, Aucho na Mauya, hilo pia linaleta ushindani mkubwa wa namba, ingawa Fei Toto ana mchango mkubwa ndani ya kikosi hicho, hilo linaheshimika,” alisema.

Tito Andrew ni beki wa zamani wa Yanga na Moro United, naye alimshauri Nabi kumtumia Aucho kucheza namba sita akisaidiana na Yanick Bangala, huku Sure Boy akipanda namba 10, ili kuikabili mechi ngumu ya Azam FC.

“Nabi anaweza akatumia mfumo wa 4-3-3 ama 4-2-3-1 yote inaweza ikampa matokeo mazuri, ingawa nina wasiwasi na Saido kama hatakuwa na ufiti wa mechi, pia tusitegemee Fei Toto kurudi sasa hivi, akimaliza hizo wiki mbili lazima ataanza kusaka ufiti kwanza, hivyo itamchukua muda mrefu kurudi kwenye moto wake,” alisema staa huyo mwenye mwili mkubwa aliyeacha soka kutokana na majeruhi ya mara kwa mara.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA MASHUJAA LEO....SIMBA WAANDALIWA MTEGO KAMA WA YANGA...