Home Habari za michezo ZILIPENDWA:…ADHABU YA CAF KWA MATOLA YAIVURUGA SIMBA…TFF WAJIFUNGIA KUJADILI…

ZILIPENDWA:…ADHABU YA CAF KWA MATOLA YAIVURUGA SIMBA…TFF WAJIFUNGIA KUJADILI…

Siku kama ya jana ikiwa ni Machi 31, lakini mwaka 2001, Chama cha


Soka Tanzania (FAT, sasa TFF) kilitangaza kwamba Aprili 9 kitakutana ili kuijadili adhabu ya wachezaji watatu wa Simba waliofungiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Kifungo cha wachezaji hao watatu, akiwamo Seleman Matola, Emmanuel Gabriel na Boniface Pawasa, ziliivuruga Simba kutokana na kuwepo kwa taarifa kwamba adhabu yao ya CAF ingeweza kutumika pia kwa michezo ya ndani.

Nyota hao walifungiwa kucheza kwa mechi za kimataifa kwa muda wa mwaka mmoja kutokana na kukutwa na makosa ya utovu wa nidhamu, lakini Katibu Msaidizi wa FAT, Michael Masanja alisema watakutana ili kujadili kwa kina na kutoa msimamo wao.

Kwa mujibu wa barua iliyotoka CAF, wachezaji hao wamefungiwa kwa kosa la kumzonga mshika kibendera katika mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Red Devils iliyofanyika mjini Kitwe Zambia.

Masanja alisema sakata hilo litajadiliwa na Kamati ya Utendaji ya FAT na hatimaye kufikia muafaka.

Hata hivyo, FAT imekuwa ikiwachanganya mashabiki wa soka hususani vinara wa ligi Simba kutokana na kutoa kauli zinazopishana.

Kwani siku chache nyuma Mwenyekiti wa FAT, Alhaj Muhidini Ndolanga alikaririwa na vyombo vya habari akisema wachezaji hao watatumikia adhabu kama hiyo kwa ligi za ndani, huku Katibu Mkuu, Michael Wambura alisema (CAF) wamefafanua kwamba adhabu hiyo ni kwa ajli ya michuano ya kimataifa tu.

Masanja na Ndolanga kwa sasa ni marehemu, huku Wambura akiwa anaendelea na mishe zake, tangu alipochoropoka kwenye kesi ya ubadhilifu na uhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabilia kabla ya kujisalimisha kwa DPP na kuachiwa huru.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA MASHABIKI KUSHINDWA KUANGALIA MECHI RWANDA, UONGOZI WA YANGA WASEMA HAYA