Rais wa heshima wa klabu ya Simba Mohammed Dewji “Mo” amewataka mashabiki wa klabu ya Simba kujitokeza kwa wingi kwenye dimba la Benjamin Mkapa siku ya jumapili kwa ajili ya kusaka tiketi ya kwenda hatua ya robo fainali kwenye mchezo dhidi ya Us Gendemarie mnamo April 3
Rais wa heshima wa Simba Sc Mohammed Dewji akizungumza leo na wachezaji na benchi la ufundi wa klabu ya Simba
Mo Dewji ameyabainisha hayo kwenye kikao cha pamoja baina ya wachezaji, benchi la ufundi sambamba na viongozi wa klabu hiyo kuelekea mchezo wa siku ya jumapili ambao utachezwa majira ya saa nne kamili usiku .
“nimetoa bonus kubwa kama wakishinda na tumezungumzia muelekeo wetu kama klabu kwa siku za mbele na niwaombe mashabiki kujitokeza kwa wingi na kushangilia kwa nguvu mwanzo mwisho, naamini itawapa nguvu wachezaji na kupambana na Inshallah tutashinda mana wachezaji wamefurahi kuniona na hakuna majeruhi na wameahidi kupambana na jumapili kupata ushindi “amesema Mo Dewji
Wakati huo huo , kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Jumanne Muliro amewahakikishia mashabiki na wapenzi wa mchezo wa soka kujitokeza kwa wingi siku ya mchezo huo kwani usalama na ulinzi utakuwa wa kutosha.
“Tunatambua mchezo huo wa shirikisho ni mchezo mkubwa ambao unahitaji mazingira ya usalama ndani ya uwanja na nje ya uwanja, kuwa ya kiwango cha juu na jeshi la polisi kanda maalumu ya dar es salaam inafuatilia kwa karibu maandalizi ya mchezo huo na jeshi limejipanga kikamilifu kuhakikisha mchezo huo utafanyika katika mazingira ya kiusalama kikamilifu nje na ndani ya uwanja “amesema kamanda Jumanne Muliro