Habari za michezo

KISA MWENDO WA JONGOO WA RONALDO…ROONEY AVUNJA UKIMYA…AICHANA MAN UTD KWA KUMSAJILI…

admin April 5, 2022 7:30 pm


GWIJI wa soka na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Uingereza Wayne Rooney ameibuka na kusema usajili wa Cristiano Ronaldo kurudi Manchester United kwa mara ya pili haukuwa sahihi.

Akifanya mahojiano na kituo cha habari cha Sky Sports cha Uingereza amedai kuwa Manchester United inahitaji kuwa na wachezaji vijana wenye njaa ili kuisaidia timu hiyo katika kipindi cha miaka 2 hadi 3.

Ronaldo amerudi kwa mara ya pili Old Trafford baada ya kuondoka mara ya kwanza mwaka 2009

“Hapana kumsajili Cristiano Ronaldo kwa mara ya pili haikuwa sahihi kwa Manchester United, ni kweli amefunga mabao na amefunga mabao muhimu katika Ligi ya Mabingwa mapema mwanzoni mwa msimu huu lakini pia amefunga hat-trick dhidi ya Totenham Hotspurs ila nadhani ukiangalia kwa siku zijazo klabu inahitaji wachezaji vijana zaidi wenye njaa ili kuweza kuisaidia timu kwa muda mrefu zaidi.”

BAADA YA TETESI KUWA NYINGI…VAN GAAL AFICHUA KUWA ANAUMWA ‘TEZI DUME’..ALIWAFICHA WACHEZAJI … MASKINI WEE..JUVENTUS WAZIDI KUPOTEANA ITALIA….WAJIKATIA ZAO TAMAA …KOCHA AJITOA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply