Habari za michezo

KUELEKEA MECHI YA KESHO….POLISI TZ WATAMBA ‘KUIPELEKEA MOTO WA KUTOSHA’ SIMBA…

admin April 9, 2022 5:30 pm


Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini amesema ubora wa kikosi chake unampa jeuri ya kuifunga Simba kesho, wakati timu hizo zitakapopambana kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza kocha huyo amesema mapumziko marefu yamewasaidia kujiandaa vizuri kwa mchezo huo, lakini pia wachezaji wake wote waliokuwa majeruhi wamepona na wapo fiti kwa ajili ya kuikabili Simba.

“Kiuhalisia mchezo utakuwa mgumu kutokana na uzoefu waliokuwa nao Simba, lakini tumejipanga vizuri kuhakikisha tunautumia vizuri uwanja wetu wa nyumbani kuifunga Simba,” amesema Malale.

Kocha huyo amesema amewaona Simba kwenye mchezo wao dhidi ya Coastal Union, ni timu ambayo ilionesha upungufu mwingi, hivyo kama watacheza kwa namna alivyowaona, basi watawafunga idadi kubwa ya mabao.

Polisi Tanzania haijawahi kuifunga Simba tangu ipande kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara, ikifungwa mechi zote za nyumbani na ugenini, kitu ambacho Malale amesema kesho wanataka kuvunja mwiko.

MAN UNITED KUVUNJA REKODI YAO YA USAJILI KWA RICE…MOYES AWAVIMBIA …ATAKA MPUNGA MREFU ZAIDI… PABLO AKAZIA ISHU YA SIMBA KUWA NA KIPORO KISA MECHI NA WASAUZI…AMWAGA ‘DATA’ HADHARANI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply