Habari za michezo

SIMBA WALIVYOPOKELEWA KWA ‘VIBE’ LA KICHAGA MOSHI…..MASTAA WOTE FULL MZUKA….

admin April 9, 2022 1:22 pm


Kikosi cha mabingwa wa Tanzania bara Simba SC kimefika salama mjini Moshi kikitokea Tanga. Tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji wao Polisi Tanzania mchezo wa Kiporo utakaochezwa Apili 10, 2022. Uwanja wa Ushirika.

Kikosi cha Simba kilicheza mchezo wa Ligi kuu jana April 07, 2022 Jijini Tanga dhidi ya Coastal Union mchezo ambao walishinda kwa ushindi wa mabao 2-1 mchezo uliochezwa katika Dimba la Mkwakwani. Mabao ya ushindi ya Wekundu wa msimbazi kwenye mchezo huo yalifungwa na Bernard Morrison na Meddie kagere.

Mabingwa hao wa Tanzania bara watacheza mchezo wa Ligi Kuu ambao ni wa kiporo dhidi ya Polisi Tanzania ambao ulipaswa kuchezwa Machi 27, 2022. Lakini ulihairishwa kutokana na kuingiliana na kalenda ya kimataifa ya FIFA kabla ya kupangwa kucheza Aprili 10, 2022 Jumapili hii. Na mchezo huu utachezwa Saa 10:00 Jioni Uwanja wa Ushirika Moshi.

AZAM WAZIDI KUPATWA NA MAJANGA….STAA WAO MWINGINE AKIMBIZWA SAUZI…. KUHUSU ISHU YA UBINGWA WA LIGI NA ASFC…NABI KAAMUA ‘KUWAPA MAKAVU LIVE’ MASTAA WAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply