Habari za michezo

LILE DILI LA GUARDIOLA KUTAKIWA NA BRAZIL KWA MSHAHARA WA BILIONI 30…KUMBE JAMAA ALISHASEMA ‘YES’…

admin April 10, 2022 9:10 am


IMERIPOTIWA kuwa Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, amepewa ofa ya mshahara wa pauni milioni 10 kwa mwaka (Sh bilioni 30 na milioni 228) ili akubali kuifundisha timu ya taifa ya Brazil.

Brazil watakabiliwa na ushindani kwa kuwa Shirikisho la Soka la Uholanzi nalo linamwania kocha huyo mwenye miaka 51.

Guardiola ana mkataba na Man City hadi 2023 na inawezekana akamaliza miaka yake ya mafanikio klabuni hapo.

Kocha wa sasa wa Brazil, Tite, tayari ameshathibitisha kuwa ataondoka katika timu hiyo baada ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, na sasa Brazil inasaka mrithi wake.

Kwa mujibu wa Marca, chama cha soka cha Brazil kinaona Guardiola ndiye mtu sahihi anayetakiwa kuinoa timu yao ya taifa.

“Hatua inayofuata ni (kuinoa) timu ya taifa kama nitapata nafasi hiyo,” alisema Guardiola mwanzoni mwa msimu huu.

Alipoulizwa kuhusiana na timu ya taifa ya Brazil, Guardiola alisema: “Ni timu nzuri ya taifa. Daima Brazil ni chaguo sahihi. Ilikuwa na itaendelea kuwa.”

KUELEKEA MECHI YA SHIRIKISHO CAF…WASAUZI WAANZA SONGOMBINGO…WAUOGOPA UWANJA WA MKAPA ETI… BAADA YA CAF KUTAKA VAR KUTUMIKA KWA MKAPA….UONGOZI SIMBA WASHINDWA KUJIZUIA…WAIBUKA NA HILI ETI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply