Habari za michezo

KISA MBINU ANAZOTUMIA PABLO…MGOSI ASHINDWA KUJIZUIA…AIBUKA NA KUFUNGUKA HAYA…

admin April 11, 2022 2:37 am


Aliyewahi kuwa Nahodha na Mshambuliaji wa Simba SC Mussa Hassan ‘Mgosi’ anaamini Kocha wa sasa wa klabu hiyo Franco Pablo Martin atavunja rekodi na kuweka rekodi yake binafsi ndani ya klabu hiyo.

Mgosi ambaye alikua Kocha wa timu ya Wanawake ya Simba SC ‘Simba Queens’ amesema Kocha Pablo ana aina tofauti ya ufundishaji na anatumia akili nyingi kufanya kazi yake, tofauti na makocha wengine wa kigenia mbao waliwahi kupita klabuni hapo.

Amesema Kocha huyo kutoka nchini Huispania pia ana misimamo ya kipekee ambayo imekua ikimsaidia kufanya kazi zake vizuri na Viongozi wa Simba SC, hali ambayo umemfanya kufikia alipo sasa, kwa kuipeleka timu hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika, na kwa upande wa Ligi anaendelea kukifanya kikosi chake kuikimbiza Young Africans kileleni.

“Ni kocha anayetumia akili nyingi kufanya kazi zake na kuyatekeleza kwa umakini mkubwa ukilinganisha na makocha wengine, pia anasimamia misimamo yake ambao imekuwa ikimpa matokeo mazuri bila ya wengi kutarajia,”

“Tangu atue na kuiongoza Simba, nimegundua hilo na pia natarajia kuona Simba SC ikifanya makubwa zaidi ikiwa chini ya Kocha huyo ila jambo kubwa ni kumpatia muda na kumuamini pasipokuingilia kazi atazidi kuipaisha timu,” amesema Mgosi.

Kocha Pablo aliajiriwa Simba SC mwishoni mwa mwaka 2021, akichukua nafasi ya Kocha Didier Gomes aliyesitishiwa mkataba wake klabuni hapo, baada ya kikosi chake kufungwa na kutolewa na Jwaneng Galaxy ya Botswana kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

RASMI…KIUNGO MNIGERIA AMUONDOA LWANGA SIMBA…HOFU YATANDA YANGA SAIDO KUAJILIWA SIMBA… KUELEKEA MECHI NA WASAUZI..HII HAPA SABABU KWA NINI MORRISON ANAWEZA KUIBEBA SIMBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply