Habari za michezo

KISA SIMBA…INJINIA HERSI AIONDOA YANGA KIMATAIFA…WADAI LENGO LAO NI NDANI KWANZA…

admin April 14, 2022 1:00 pm


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Hersi Said amesema kwamba licha ya baadhi ya watu kuanza kuipigia hesabu michuano ya kimataifa msimu ujao, hilo kwasasa sio kipaumbele chao bali wanachokiwaza ni kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara ambao pia unawaniwa na Simba SC wakiwa ni mabingwa watetezi.

Hersi ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM amesema kuwa mara zote yeye huwa anafikiria kilicho mbele yake na anachofahamu ni kwamba wana Yanga wote wana kiu ya kutwaa Ubingwa wa NBC.

”Kama nilivyosema awali ni kuwa tulikuwa tunaijenga klabu yetu ili tufanikiwe kwenye mashindano ya ndani, ukishalifanikisha hilo ndipo tutaweza kupambana kwenye michuano ya kimataifa na hilo lipo katika mipango yetu” Hersi Said Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM.

Katika hatua nyingine Hersi amesema wanajiandaa kwa ajil ya kuwakabili watani zao wa jadi Simba katika mchezo wa tarehe 30 ambao utatoa taswira pana juu ya safari yao ya ubingwa msimu huu.

WAKATI MAWAZO YA SIMBA YAKIWA KWA WASAUZI KWANZA…YANGA WAIBUKA NA KUTOA MSIMAMO WAO… AZAM WATINGA KIBABE NUSU FAINAL KOMBE LA SHIRIKISHO…YAWAKUNGU’UTA WABABE WA SIMBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply