Uongozi wa Klabu ya Mtibwa Sugar umekanusha kuwa beki wake Abdi Banda kuhusika na taarifa zinazowahusisha wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa,Wekundu wa msimbazi Simba kuwa wanatumia mbinu zisizo za kimpira kupata matokeo kwenye mechi zake za kimataifa kwenye Uwanja wake w
Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Mtibwa, Saad Kawemba amesema haikuwa taarifa nzuri na wao kama Viongozi walichukua hatua ya kuwasiliana na baadhi ya Viongozi wa Simba ili kuwapa muda wa kulifanyia uchunguzi suala hilo, na taarifa za awali zimeonyesha kuwa Abdi Banda hakuhusika na sakata hilo na bado wanaendelea kufuatilia kujua aliyeanzisha uzushi huo alikuwa na lengo lipi.
”Ni jambo baya kupita kiasi, sisi kama Viongozi tulipoliona tuliwasiliana na baadhi ya Viongozi na klabu inayotajwa kufanya vitendo visivyo vya kimpira na tukawaomba watupe nafasi tufanye uchunguzi na wao wakitusaidia , lakini tuliongea na Kocha na watu wa karibu ili kumuuliza mchezaji iwapo yeye ndiye anayehusika na taarifa za awali Abdi Banda amekanusha kuhusika na suala hilo hivyo yupo na timu anaendelea na mazoezi”Mtendaji Mkuu wa Mtibwa Sugar, Saad Kawemba akizungumzia tetesi za beki wao kuizungumzia Simba kuwa inatumia mbinu chafu kupata matokeo kwenye mechi zake za kimataifa.
Banda alinukuliwa akitoa taarifa kwenye mtandano wa michezo mashughuli huko nchini Afrika Kusini akiwatahadharisha wapinzani wa Simba, orlando Pirates kujiandaa na mbinu chafu za wawakilishi hao wa nchi kimataifa kwakuwa ni hodari kutumia njia ambazo ni ngumu kwa wao kupata ushindi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.