Habari za michezo

A-Z NAMNA SIMBA WALIVYOWACHACHAFYA WASAUZI KWA MKAPA JANA…MORRISON HANA DENI….

admin April 18, 2022 9:18 am


KLABU ya soka ya Simba imefanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Klabu ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Bao la Simba limefungwa na mlinzi wake wa kulia Shomari Kapombe katika dakika ya 68 kwa mkwaju wa penati kufuatia mshambuliaji wa timu hiyo Bernard Morrison kufanyiwa madhambi katika eneo la penati.

Simba ilitawala mchezo kwa asilimia 55 huku Orlando Pirates wakionekana kucheza kwa tahadhari ya kutokuruhusu mabao ya ugenini.

Mechi ya marudiano inatarajiwa kuchezwa Jumapili ya wiki ijayo Aprili 24 jijini Johannesburg Afrika Kusini ambako Simba itahitaji sare ya aina yoyote ili iweze kufuzu katika hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.

SIMBA YA CAF RAHA TUPU…MO DEWJI AIBIPU YANGA…WAARABU WATIA MKONO DILI LA YANGA…. MAMBO NI MOTO USAJILI MPYA YANGA….INJINIA HERSI ATUA RWANDA KUFUATA KIFAA CHA KAZI KAZI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply