Home Habari za michezo BAADA YA KUONA TAARIFA ZAKE ZA KUWA MAJERUHI ZIPO NYINGI..CHICO AIBUKA NA...

BAADA YA KUONA TAARIFA ZAKE ZA KUWA MAJERUHI ZIPO NYINGI..CHICO AIBUKA NA KUVUNJA UKIMYA..


Winga mpya wa Yanga ambaye hajaonyesha makeke kama ilivyotarajiwa tangu asajiliwe kutoka TP Mazembe, Chico Ushindi amepiga mkwara kwa sasa yupo fiti na anasubiri kuliamsha Ligi Kuu Bara.

Chico alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha, huku kocha wake wa viungo akifichua pia kutokuwa fiti ndio sababu kubwa ya kushindwa kuwika kikosini na anajua ana deni kwa wanayanga.

Akizungumza Chico alisema ameshapona majeraha yake na anachosubiri ni kuona anapewa nafasi ya kuonyesha makali yake kwenye mechi zijazo akitarajiwa kuanza na Namungo kabla ya kuimaliza Aprili kwa kuivaa Simba.

Winga huyo alikuwa akiuguza jeraha la mguu na kuna wakati alipona na kuanza kucheza, lakini akajitonesha na kuendelea kuwa nje ya kikosi, lakini kwa sasa yupo fiti na anataka nafasi ya kucheza kuonyesha makali yake.

“Najua watu wanauliza kuhusu mimi, niwaambie nimeshapona sasa nadhani kuanzia mechi na Namungo kama kocha ataniweka kwenye mipango mtaniona. Ninajua nina deni kwa mashabiki wa klabu hii,” alisema Chico.

Akizungumzia upande wa ushindani wa namba akichuana na mawinga wenzake kama Denis Nkane, Farid Mussa, Dickson Ambundo na Deus Kaseke, Mkongomani huyo alisema amekuja Tanzania kupambana na wajibu wake kuipigania namba.

Tangu atue Jangwani, Chico amecheza mechi tatu tu za Ligi Kuu, moja akianza na mbili akitokea kwenye benchi., ukiwamo ule wa Polisi Tanzania alipoingia dakika 78 kumpokea Jesus Moloko na ule wa Mbeya City ulioisha kwa suluhu alipoingizwa dakika ya 82.

SOMA NA HII  IRAHISISHE WIKIENDI YAKO KWA MTONYO WA MERIDIANBET...ODDS HAPA NI UHAKIKA NA ZAKUSHIBA......