Home Habari za michezo CAMEROON: MABASI 89 YALIYOTUMIWA NA TIMU ZA TAIFA WAKATI WA AFCON...

CAMEROON: MABASI 89 YALIYOTUMIWA NA TIMU ZA TAIFA WAKATI WA AFCON HAYAJULIKANI YALIPO…


Miezi miwili baada ya kumalizika kwa Michuano ya Kombe la Afrika (AFCON), mabasi 89 kati ya 90 yaliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kusafirisha timu za Mataifa shiriki hayajulikani yalipo huku basi 1 lililotumiwa na Timu ya Taifa ya Cameroon ndio linajulikana lilipo.

Kumeibuka tetesi kuwa Wafanyakazi waliohusika katika usimamizi wa michuano hiyo hawajakamilishiwa malipo yao.

Mamlaka husika hazijatoa tamko rasmi kuhusu tetesi hizo.

Tabia hii ya kujimilikisha mali ama vitu mara baada ya tukio fulani imekuwa ikikithiri zaidi kwenye jamii ya kiafrika, ambapo wengi huzani pengine kwa kuwa walikabidhiwa dhamana ya kuvihodhi wanahaki ya kujimilikisha uhalali wa mali hizo.

Hii inachukuliwa kama moja ya tabia mbovu zaidi kwa jamii iliyokosa ustarabu na kuheshimu mali za jamii, ambapo pia kwa lugha nyingine huitwa ‘ufisadi’ na uroho wa mali za umma.
SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA