Home Habari za michezo BAADA YA KUPOKEA KICHAPO CHA JANA…MAN UNITED WAINGIA RASMI KWENYE REKODI HII...

BAADA YA KUPOKEA KICHAPO CHA JANA…MAN UNITED WAINGIA RASMI KWENYE REKODI HII YA AJABU…


Baada ya kukubali kichapo cha magoli 4 kwa sifuri kutoka kwa Liverpool usiku wa jana, sasa klabu ya Manchester united ndio timu iliyoruhusu kufungwa magoli mengi zaidi na Liverpool katika historia ya ligi kuu ya England kuliko mpinzani mwingine yoyote wakifungwa jumla ya magoli 74.

Vile vile Liverpool pia imekua timu ya kwanza kufunga magoli tisa dhidi ya Manchester United katika michezo miwili ya msimu mmoja, baada ya kushinda magoli matano kwa sifuri katika mchezo wa mzungo wa kwanz akatika dimba la Old Trafford.

Na nyota wa klabu hiyo Mohammed Salah sasa amekua mchezaji wa kwanza katika ligi ya England kufunga magoli matano dhidi ya Manchester United katika msimu mmoja, na pia ni mchezaji wa pili kufunga magoli na kutoa pasi za magoli kwenye michezo yote miwili wa nyumbani na ugenini katika msimu mmoja dhid ya mashetani hao wekundu, baada ya Mesut Ozil kufanya hivyo akiwa Arsenal msimu wa mwaka 2015/16.

Wachambuzi na manguli wa zamnai wa Manchester united wameonyesha kuchukizwa na matokeo hayo huku Gary Neville akikosoa vikali kuhusu umiliki wa familia ya Glazer, wakati Roy Kean akisema hii siyo Manchester united aliyoichezea yeye maana haikua na kiwango kibovu kiasi hiki.

Naye kocha wa muda wa klabu hiyo Ralf Rangnick amesema kipigo cha jana moja kati ya vipo vya aibu sana na kuna uwekezaji mkubwa unatakiwa kufanyika ili kuiunda upya United na kwa mpango uliopo sasa wanatarajia kusajili wachezaji kadhaa majira ya kiangazi mwaka huu.

Lakini kitu kingine alichosisitiza Rangnick ni kwamba haitoshi tu kusajili wachezaji wapya, lakini pia sasa ni muda muafaka wa kufikiria ni wachezaji wangapi wanapaswa kuondolewa klabuni hapo ukiacha eneo la goli kipa ambalo linaonekana kuridhidsha kwa viwango vya magoli kipa wote walio nao.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA MECHI NA WATUNISIA LEO NI NGUMU...NABI KAONA ISIWE TABU...AITAJA SIMBA...