Home Habari za michezo KUELEKEA KARIAKOO DABI….NABI AJIFUNGIA KUMSOMA SAKHO…AITAZAMA MWANZO MWISHO MECHI YA JUZI…

KUELEKEA KARIAKOO DABI….NABI AJIFUNGIA KUMSOMA SAKHO…AITAZAMA MWANZO MWISHO MECHI YA JUZI…


BENCHI la Ufundi la Yanga pamoja na wachezaji wa timu hiyo, waliutumia mchezo wa Robo Fainali wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba dhidi ya Orlando Pirates, kuangalia mbinu za watani wao wa jadi, Simba.

Katika mchezo huo uliomalizika kwa Simba kushinda bao 1-0, waliwatumia wachezaji wake wote mastaa akiwemo Ousmane Sakho ambaye ndiyo tishio hivi sasa.

Hiyo ni katika kujiandaa na Kariakoo Dabi itakayowakutanisha Simba dhidi ya Yanga Aprili 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Kwa mujibu wa taarifa, kocha huyo akiwa kambini Avic Town, Kigamboni, Dar, alikuwa makini kuangalia mchezo huo kwa lengo la kuangalia ubora na udhaifu wa Simba.

Aliongeza kuwa, dakika hizo 90 zimetosha kwa Nabi kujua upungufu na wachezaji hatari wa kuchungwa.

“Wachezaji na benchi la Ufundi la Yanga wote walikuwa wakiufuatilia mchezo wa leo (juzi) kati ya Simba na Pirates.

“Kocha ndiye aliyetoa maagizo hayo, kikubwa kocha alikuwa akitaka kuwaona na kuwafuatilia wachezaji hatari wenye madhara kwa ajili ya kuwazuia watakapokutana,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Nabi kuzungumzia hilo, alisema: “Kabla ya mchezo dhidi ya Simba tuna mechi nyingine ya ligi na Namunguo ambao nao muhimu tunahitaji pointi tatu, hivyo kwa sasa akili zangu zinaiwaza mechi hiyo, lakini ni muhimu kupata ushindi michezo yote miwili ijayo,” alisema Nabi.

SOMA NA HII  HIZI HAPA REKODI KIBAO AMBAZO LIVERPOOL WALIWEKA JANA BAADA YA KUFUZU FAINAL UEFA...