Habari za michezo

PENATI YA KAPOMBE DHIDI YA WASAUZI YATOA SOMO LIGI KUU…MABEKI WAFUNGUKA WALICHONASA….

admin April 21, 2022 7:45 am


Umahiri na ujasiri aliouonyesha beki wa Simba, Shomari Kapombe kupiga penalti muhimu ya bao pekee dhidi ya Orlando Pirates, umetoa somo kwa baadhi ya mabeki kujifunza kitu kwake.

Mbali na penalti ya juzi ya mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa Mkapa, ya kwanza alifunga dhidi ya ASEC Mimosas, akitupia bao la pili lililowarejesha mchezoni na kumaliza dakika 90 kwa ushindi wa mabao 3-1.

Beki wa Mtibwa Sugar, Ibrahim Ame alisema ugumu wa penalti alizopiga Kapombe CAF, ulitokana na Simba kupata matokeo ya ushindi na kama angekosa huenda timu isingefika hapo.

Adeyum Saleh, beki wa Geita Gold alimsifu akisema:

“Penalti kama zile zinahitaji kujiamini maana zinakuwa zimebeba hatima za furaha ya mashabiki ndiyo maana wengine wanazimia na wengine kupoteza maisha.”

ADEBAYOR AITAJA SIMBA….YANGA NA MWAMNYETO WAMEFIKIA HAPA…SIMBA YAWAANDALIA SAPRAIZI WASAUZI… WAKATI MAYELE AKIZIDI KUTETEMA YANGA…BONIFACE AMBANI AIBUKA NA KUMLIPUA…AOMBA KAZI YANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply