Habari za michezo

MCHEZA TENNIS NA DEREVA WA LANGALANGA WAUNGANA KUTAKA KUINUNUA CHELSEA…DILI LAO LIKO HIVI…

admin April 22, 2022 11:21 am


Dereva wa langalanga Lewis Hamilton na nyota wa tennis Serena Williams wameungana na mwekezaji Sir Martin Broughton kutaka kuinuna klabu ya Chelsea iliyopo sokoni hivi sasa.

Hamilton ambaye ni bingwa mara saba wa dunia wa michuano ya langalanga sambamba na Serena Williams ambaye ametwaa mataji 23 ya Grandslam kwenye mchezo wa tennis wanaungana na rais wa chama cha riadha duniani Sebastian Coe ambaye anamuunga mkono tajiri Sir Broughton

Broughton pia anaungwa mkono na wamiliki wenza wa klabu ya Crystal Palace Josh Harris na David Blitzer huku akipata msaada mkubwa wa kifedha kutoka kwa wawekezaji wengine kama Michael Klein na Lord Coe huku Hamilton na Serena Williams hawatahusika na maamuzi yoyote kwenye mambo ya soka iwapo tenda ya Sir Broughton itashinda dili la kuinunua klabu ya Chelsea .

KAPOMBE AWA GUMZO AFRIKA KUSINI….MASHABIKI WA KAIZER CHIEFS, MAMELOD WAOMBA JEZI ZA SIMBA… KIUNGO WA BURUNDI AJIPIGIA DEBE YANGA…AFUNGUKA ATAKAVYOKIWASHA AKIPANGWA NA FEI TOTO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply