Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA SIMBA..KAZE AVUNJA UKIMYA YANGA….JULIO AKUBALI YAISHE..ADAI YANGA NI BABA...

KUELEKEA MECHI NA SIMBA..KAZE AVUNJA UKIMYA YANGA….JULIO AKUBALI YAISHE..ADAI YANGA NI BABA LAO…


Yanga imejihakikishia kuivaa Simba katika mchezo wa Aprili 30 ikiwa kileleni mwa msimamo kwa pointi 13 dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili.

Ushindi wa Yanga wa mabao 2-1 dhidi ya Namungo katika mchezo wa Jumamosi wa Ligi Kuu Tanzania Bara imeifanya miamba hiyo kuisubiri Simba bila presha baada ya kushinda katika michezo sita migumu zaidi katika ligi.

Ushindi dhidi ya Coastal Uniion (2-0), Polisi Tanzania (1-0), Geita Gold (1-0), Mtibwa Sugar (2-0), Kagera Sugar (3-0), Azam FC (2-1) na Namungo (2-1) uliifanya yanga kujiimarisha katika uongozi wa ligi msimu huu.

Akizungumza baada ya mchezo huo wa Jumamosi, kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze alisema sasa wanaweza kuanza kuufikiria mchezo wa derby kwani ndiyo unaofuata na wanahitaji kuendeleza ushindi mfululizo.

Kaze alisema ilikuwa ngumu kwao kuanza kuifikiria Simba wakati kulikuwa na mchezo mwingine mgumu wa Ligi Kuu, ambao walitakiwa kupata pointi tatu kwa ajili ya kuendelea kutafuta lengo lao.

“Isingekuwa rahisi kuanza kuifikiria mchezo wa Aprili 30 (dhidi ya Simba) wakati kuna mchezo wa Aprili 23, isingekuwa pia heshima kwa Namungo, wana timu nzuri ndiyo maana tulikuwa hatujawahi kuwafunga.

“Lakini sasa tunaweza kuanza kuifikiria Simba maana ndiyo mchezo wetu unaofuata, mazoezi na mbinu zote ni kwa ajili ya Simba, tunahitaji kushinda kila mchezo ikiwa tunataka kusimamia lengo kuu la msimu huu,” alisema Kaze.

Kocha wa Namungo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ aliipongeza Yanga kwa ushindi huo akisisitiza kuwa mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu wanastahili kuwa kileleni kutokana na kuwa na timu nzuri msimu huu.

“Ni timu nzuri, tulihitaji kuibuka na ushindi katika mchezo huu, tulipoteza umakini na kuruhusu nafasi ambazo wenzetu wametumia vizuri. Ukiangalia timu tuliyocheza nayo inaongoza katika msimamo, haikuwa jambo la bahati kwani wana timu nzuri,” alisema Julio.

Yanga itakutana na Simba ikiwa na pointi 13 zaidi ya Simba yenye pointi 41 katika nafasi ya pili, huku mabingwa hao wa zamani wakisisitiza kuibuka na ushindi katika kila mchezo ili kutangaza ubingwa mapema.

SOMA NA HII  HATIMA YA MAYELE NA YANGA IKO HIVI...ATAKA MSHAHARA WA MILI 53 KWA MWEZI...ADA YA USAJILI BIL 1...

Shabiki wa Yanga, Haruna Chowe alisema ushindi dhidi ya Namungo umeshusha presha iliyopo kwa mashabiki wengi kuelekea mchezo wa Aprili 30, dhidi ya Simba.

Chowe alisema kwa Yanga kuibuka na ushindi ghuo umekifanya kikosi chao kuwa na wakati mzuri wa kuwazia mchezo ujao bila presha ya kupungua kwa pointi chini ya 10.

“Hii imekuwa raha zaidi, kwani hata kama Simba itatufunga au kupata sare, pengo la pointi haliwezi kuwa chini ya 10 na Simba ina kiporo kimoja tu, hivyo tunaamini tutakuwa na wakati mzuri zaidi yao katika mchezo huo,” alisema Chowe.

Simba ilikuwa na mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shieikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates nchini Afrika Kusini, jana, hivyo baada ya mchezo huo itarudi kujiandaa dhidi ya Yanga.