Hatua ya Nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya inatarajiwa kuanza rasmi majira ya saa 4 usiku wa leo kwa mchezo mmoja kupigwa Kwenye dimba la Etihad, ambapo Manchester City watakuwa uwanjani kuwakabili Mabingwa wa kihistoria wa michuano hii Real Madrid.
Timu hizo zimekutana mara 6 kabla ya mchezo wa leo, Manchester City akishinda michezo miwili, na Real Madrid akishinda michezo miwili huku michezo mingine miwili ikimalizika kwa sare. Mara ya mwisho timu hizi zinakutana msimu wa 2020/2021 hatua ya 16 bora na Real Madrid alipoteza mechi zote mbili mbele ya City.
Katika mchezo wa leo Manchester City wanatarajiwa kuwakosa Joao Cancelo na Kylie Walker huku Real Madrid wakitarajiwa kumkosa Casemiro.
Pep Guardiola sasa anaenda kumaliza miaka 10 ya maumivu katika mashindano ya ligi ya mabingwa barani ulaya, na hajashinda Ligi ya Mabingwa tangu mwaka 2011. Huu ni msimu wa 11 wa Manchester City kwenye Ligi ya Mabingwa barani ulaya wamekuwa wakishiriki katika hatua ya makundi kila msimu tangu 2011/12 na sasa wamefika hatua ya mtoano katika misimu tisa mfululizo.
Hata hivyo matarajio ya klabu hiyo yenye maskani yake jijini Manchester nchini England kwa muda mrefu hayajatimizwa, kwani msimu uliopita City walipoteza mchezo wa fainali ya michuano hiyo dhidi ya chelsea kwa kupoteza kwa bao 1 kwa 0 nchezo uliopigwa katika dimbala dragao mjini Porto.