Habari za michezo

KIMENUKAAH…WASAUZI WAISHITAKI SIMBA CAF KWA KUCHOMA UWANJA WAO MOTO…

admin April 29, 2022 7:00 am


MTENDAJI MKUU wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchini Afrika Kusini Tebogo Motlanthe amesema kitendo cha Klabu ya Simba kutoka Tanzania kuchoma kitu katikati ya Uwanja ni jambo la aibu na si la kiuanamichezo.

Motlanthe amesema kitendo hicho hakikubaliki na tayari kama Shirikisho tayari wameandika barua kwenda Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuona hatua stahiki zinachukuliwa.

Klabu ya Simba ilitolewa na Klabu ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-3 baada ya timu hizo kufungana bao 1-1 katika michezo yote miwili ya hatua hiyo ya mtoano.

UTAMU WA KLOPP WAUPAGAWISHA UONGOZI LIVERPOOL….WAAMUA LIWALO NA LIWE… KUELEKEA KARIAKOO DABI KESHO…HUU HAPA UTAMU AMBAO HUPASWI KUUKOSA …

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply