Habari za michezo

KUELEKEA MECHI YA LEO….AUSSEMS AIUA SIMBA MAPEMAA…AIBETIA YANGA USHINDI WA KISHINDO…

admin April 30, 2022 12:05 pm


Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Aussems, raia wa Ubelgiji, ameweka wazi kuwa kwa upande wake, anaona Yanga wana nafasi kubwa katika mchezo wa leo Jumamosi dhidi ya Simba kutokana na kubebwa na rekodi ya matokeo ya mechi zao zilizopita, tofauti na wapinzani wao.

Aussems ambaye kwa sasa ni Kocha wa AFC Leopards ya Kenya, ametoa kauli hiyo kuelekea katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ambao utazikutanisha Simba na Yanga.

Aussems amesema; “Nadhani kwangu naona Yanga wanayo nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo kutokana na rekodi ya mechi za mwisho kwenye ligi, tofauti na Simba ambao wametoka kupata sare halafu wameondolewa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika. Inaonyesha kwao kukata tamaa japokuwa lolote linaweza kutokea

Patrick Aussems alifukuzwa Simba mara baada ya kushindwa kusimamia masuala ya kinidhamu kwa wachezaji pamoja na kutoifikisha timu hiyo kwenye nusu Fainal ya klabu bingwa Afrika, ambapo Simba walitolewa na TP Mazembe.

YANGA vs SIMBA….LIWALO NA LIWEE…CHAMA, MORRISOM MZUKA JUU…MO AMALIZA…. BAADA YA YANGA KUILALAMIKIA SIMBA KWA KUISUSA MECHI YA LEO…AHMED ALLY KAWAJIBU HAYA KIBABE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply