Home Habari za michezo BAADA YA KUAMBIWA HAYUPO KWENYE MCHEZO WA LEO..YACOUBA AVUNJA UKIMYA YANGA…AIBUKA NA...

BAADA YA KUAMBIWA HAYUPO KWENYE MCHEZO WA LEO..YACOUBA AVUNJA UKIMYA YANGA…AIBUKA NA HILI…


BAADA ya kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi kuthibitisha kumkosa Yacouba Sogne kwenye mchezo wa leo straika huyo ameibuka na kusema wana kikosi bora na wanahitaji ubingwa bila kupoteza mechi.

Yanga itakuwa mwenyeji kwenye mchezo huo unaopigwa leo kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam timu hizo zikiwa na kumbukumbu ya kugawana pointi mzunguko wa kwanza baada ya kutoka suluhu.

Yacouba alisema anapitia wakati mgumu kuishia kuwatazama wenzake wakicheza lakini anapata furaha kutokana na matokeo yanayopatikana huku akithibitisha kuwa utakuwa mchezo mgumu na wa ushindani.

“Nimekaa nje ya uwanja msimu mzima sasa kutokana na kusumbuliwa na majeraha, timu haijatetereka, nafurahia hilo lakini napitia wakati mgumu sana kwani nimeshindwa kufanya kile kilichotarajiwa na wengi,” alisema na kuongeza;

“Naipa nafasi kubwa Yanga kuibuka na ushindi Jumamosi kutokana na ubora wa timu sambamba na malengo waliyonayo wachezaji kuhakikisha wanatwaa taji msimu huu bila kufungwa, mchezo utakuwa mgumu na wa ushindani Yanga ni bora na ndio wataibuka na ushindi.” alisema.

Alisema amekosekana kwenye mechi zote mbili ya mzinguko wa kwanza timu yake ikiambulia sare na hatakuwa miongoni mwa wachezaji watakao cheza Jumamosi lakini ana imani kubwa na mastaa watakaocheza huku akikiri kuwa timu yake ni bora kila idara.

“Unajua hata mzunguko wa kwanza Yanga ilishindwa kupata matokeo kutokana na timu kutokukaa pamoja muda mrefu ili kutengeneza maelewano lakini walionyesha uwezo sasa timu ishakaa pamoja muda mrefu na inapata matokeo kwa kucheza kwa kuelewana hakuna kitakachowazuia kupata matokeo,” alisema na kuongeza;

“Wachezaji wapo kwenye hali nzuri wanatamani kucheza na kupata matokeo ili kufikia lengo lao la kutwaa taji msimu hii ambalo ni wazi lipo upande wao hii ni jitihada za wachezaji na benchi la ufundi sitacheza lakini nipo pamoja nao kwa kila hatua.”

Yacouba aliongeza kuwa tangu ametua Yanga msimu huu ameshuhudia ubora mkubwa wa wachezaji waliosajiliwa na kuimarika kwa viwango kwa wachezaji waliokuwepo.

“Mashabiki washindwe wenyewe kuja kushuhudia burudani ya kutosha Jumamosi Yanga ya msimu huu ni imara na ya mafanikio kuna vipaji vipya na kuna kuimarika kwa vipaji vilivyokuwepo.” alisema mkali huyo kutoka Burkina Faso.

SOMA NA HII  KISA SIMBA...DJIGUI DIARA AWEKWA KANDO YANGA....NABI AFUNGUKA A-Z MAMBO YALIVYO...AMTAJA SAKHO....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here