Home Habari za michezo BAADA YA KUTUA CHATO…KMC WATEMBELEA KABURI LA MAGUFULI…WAWEKA HISTORIA YA MAPOKEZI…

BAADA YA KUTUA CHATO…KMC WATEMBELEA KABURI LA MAGUFULI…WAWEKA HISTORIA YA MAPOKEZI…


Wachezaji, Viongozi pamoja na Benchi la ufundi KMC FC leo wamezuru katika kaburi la hayati Dokta John Joseph Pombe Magufuli nyumbani kwake Wilayani Chato Mkoani Geita ikiwa nisehemu ya kutambua na kuenzi mchango wake katika sekta ya michezo alioufanya enzi ya uhai wake.

KMC FC ambayo imeweka kambi Wilayani Chato tangu Aprili 18 mwaka huu ikiwa ni mara baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar,uliopigwa Aprili 17 katika uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera, inaendelea kutambua mchango mkubwa ambao Hayati Dk. Magufuli aliounesha kwenye sekta hiyo enzi ya uhai wake.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni, ikiwa Chato imefika pia ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi na kupata mapokezi mazuri pamoja na ushirikiano mkubwa ikiwa ni pamoja na kufanikisha kufika nyumbani kwa hayati Dk. Magufuli lakini pia kutumia uwanja wa Magufuli unaomilikiwa na Wilaya hiyo kufanya kwa ajii ya kufanya mazoezi.

“ KMC tunatambua mchango mkubwa ambao hayati Dk. Magufuli aliufanya enzi ya uhai wake katika sekta hii ya michezo, hivyo ndio mana tukaona wakati huu ambao Timu ipo huku kanda ya ziwa tufike nyumbani kwake kuzuru pamoja na kusalimia familia yake, lakini pia kufika kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi ambapo kimsingi tumepata mapokezi makubwa na tunawashukuru kwa hilo.

Lakini pia wakazi wa Chato wameonesha kufurahishwa na uwepo kwa KMC, kwani wakati wamzoezi wamejitokeza kwa wingi kuwasapoti wachezaji nah ii kwetu kama Timu tumechukua kama sehemu ya kutambua mchango wao kwetu na hivyo kuahidi kutoa ushirikiano mkubwa pindi tutakapokuja huku kwa mara nyingine.

Hata hivyo KMC FC inaendelea kujiimarisha kuelekea katika mchezo muhimu wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania dhidi ya Geita utakaopigwa siku ya jumamosi ya Aprili 23 katika Uwanja wa Magogo saa 16:00 jioni.

Imetolewa leo Aprili 21

Na Christina Mwagala

Afisa Habari na Mawasiliano wa KMC FC- Chato.

SOMA NA HII  BAADA YA KUFUNGWA JANA..KOCHA WA NAMUNGO ASHINDWA KUJIZUIA...ALIPUKA MAPYA..AITAJA SIMBA...