Home Habari za michezo BALAMA ARUDI KWA KASI YA KIMBUNGA YANGA…AWAPIGA MKWARA WENZAKE..KAZE KUMPELEA ‘UBUYU’ NABI..

BALAMA ARUDI KWA KASI YA KIMBUNGA YANGA…AWAPIGA MKWARA WENZAKE..KAZE KUMPELEA ‘UBUYU’ NABI..


Kiungo Mapinduzi Balama amerejea kwa kishindo uwanjani baada ya juzi kati kutupia bao moja kambani katika mechi ya kirafiki dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar, kisha kumuomba Kocha Nasreddine Nabi ampe nafasi ya kuliamsha kikosini.

Balama aliyekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi na katika pambano hilo dhidi ya Mafunzo, alicheza kwa dakika 59 na kufunga bao moja, kitu kilichompa faraja na kusema anahitaji muda zaidi ili arudi kwenye moto wake.

Hata hivyo, kauli ya Balama imekuja wakati Yanga ikiwa imejaza mafundi katika eneo hilo la kati, huku nyota wanaotumika kwa sasa kuonekana moto zaidi akiwamo Feisal Salum ‘Fei Tito’ na Saido Ntibazonkiza waliochangia mabao 19 – Saido akifunga mabao sita na kuasisti tano na alikiri Yanga ya sasa imeshiba.

Balama alisema anatambua malengo ya klabu sasa ni kusaka ubingwa na amekubali kukaa kwake nje kwa muda mrefu kumetoa nafasi kwa wenzao kukiwasha, ila anaamini amerudi na anahitaji mechi zaidi kujenga kujiamini.

“Yanga inahitaji matokeo kila mchezo kutokana na kuwa na uchu wa mataji, uwezo wa kufunga ninao lakini bado nahitaji muda wa kurudisha uwezo wangu nimekaa nje ya uwanja msimu mmoja na nusu sasa, najua wanaocheza nafasi yangu ni bora na wanastahili kuanza, ila nikimaliza na mmoja wao sio itanisaidia,” alisema.

Mbali na nafasi ya namba kumi anayocheza Balama pia anaweza kucheza kama winga na kocha msaidizi, Cedric Kaze alisema: “Soka ni mchezo wa wazi kila mmoja ameona na kocha mkuu atafikishiwa taarifa namna wachezaji walivyoonyesha uwezo na kazi itabaki kwake kuchagua wa kumpanga ili kwenda na kasi ya timu.”

SOMA NA HII  KISA ISHU YA SAIDO NA AMBUNDO KUSIMAMISHWA...MAYELE, SHABANI DJUMA WAJILIPUA YANGA...'WAMFESI' NABI BILA UOGA..