Home Habari za michezo BUMBULI – HATA TUKIFUNGWA NA SIMBA TUTAENDELEA KUWA NA FURAHA TU…

BUMBULI – HATA TUKIFUNGWA NA SIMBA TUTAENDELEA KUWA NA FURAHA TU…


Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Young Africans Hassan Bumbuli amesema hata kama ikitokea kikosi chao kitapopteza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba SC, hawatakua na majonzi zaidi ya kufikiria taji la Ligi Kuu msimu huu 2021/22.

Young Africans itaikabili Simba SC Jumamosi, Uwanja wa Benjamin Mkapa saa kumi na Moja Jioni, huku ikiwa klabu pekee inayoshiriki Ligi hiyo ambayo haijapoteza mchezo msimu huu 2021/22.

Bumbuli amesema mpaka sasa klabu yao ina mtaji mkubwa wa alama na dhamira yao ni kuendelea kukusanya alama nyingine tatu dhidi ya Simba SC Jumamosi (April 30), hivyo wapo tayari kwa hilo japo inaweza kutokea mambo yakawa tofauti.

Amesema hakuna timu inayokwenda Uwanjani ikiwa na lengo la kupoteza mchezo, lakini kinachotokea baada ya dakika 90 ni sehemu ya matokeo ambayo yanaweza kuwa furaha upande wao ama huzuni kwa wapinzani, lakini pia inaweza kuwa huzuni kwao na furaha kwa wapinzani.

“Tumejipanga kushinda mchezo wetu wa Jumamosi, tunaamini tuna kikosi kizuri sana, jambo ambalo tumelifanya msimu huu ni kukusanya alama nyingi zaidi ambazo zitatusaidia hata tukipoteza mchezo bado tutaendelea kuwa na lengo la kutwaa Ubingwa.”

“Tunajua Soka lina matokeo ya aina tatu, lakini kwetu sisi tunatangalia kushinda kwanza ili kuendelea kukusanya alama, ikitokea mambo mengine bado itakua ni faida kwetu kwa sababu mtaji wa alama tulio nao ni mkubwa na hata Simba SC wanalijua hilo.” amesema Bumbuli

Mara ya mwisho timu hizo Kongwe zilipokutana msimu huu 2021/22, zilitoshana nguvu kwa kutoka sare ya 0-0, huku mwanzoni mwa msimu huu katika mchezo wa Ngao ya Jamii Simba SC ilipoteza kwa kufungwa 1-0.

Simba SC inakwenda kukutana na Young Africans huku ikiwa na asilimia kubwa ya kuutema ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu, kufuatia kuachwa kwa alama 13 katika msimamo wa Ligi Kuu hadi sasa, huku timu hiyo ikicheza michezo 19.

Young Africans iliyocheza michezo 20 inaongoza msimamo ikiwa na alama 54, ikifuatiwa na Simba SC yenye alama 41, huku Namungo FC ikiwa nafasi ya tatu kwa kufikisha alama 29 na Azam FC ipo nafasi ya nne kwa kumiliki alama 28.

SOMA NA HII  GAMONDI AFANYA KOSA HILI...MASHUJAA KUKUMBANA NA HILI...ISHU NZIMA HII HAPA