Home Habari za michezo FEI TOTO AJITABIRIA HAYA MECHI YA YANGA vs SIMBA…AMKABIDHI KAZI ‘SURE BOY’...

FEI TOTO AJITABIRIA HAYA MECHI YA YANGA vs SIMBA…AMKABIDHI KAZI ‘SURE BOY’ MECHI YA AZAM…


KIUNGO fundi wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ametoa maneno mazuri kwa mashabiki wa timu hiyo akiwaambia kukosekana kwake uwanjani kwa wiki mbili siyo tatizo, kwani wapo viungo wengine bora kama yeye.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni siku chache tangu kiungo huyo aondolewe kwenye kambi ya Taifa Stars iliyokuwa ikijiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudan uliochezwa juzi Jumanne kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Kiungo huyo aliondolewa kambini baada ya kupata majeraha ya goti ikiwa ni siku chache tangu watoke kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Fei Toto alisema anaamini atapona na atarejea uwanjani mapema tayari kwa ajili ya kuipambania timu hiyo inayowania ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Fei Toto alisema licha ya kukosekana katika mchezo ujao wa ligi dhidi ya Azam FC, lakini anaamini wapo viungo watakaocheza vizuri na kuziba pengo lake ambao ni Salum Aboubakar ‘Sure Boy’, Khalid Aucho, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ na Yannick Bangala.

Aliongeza kuwa, mara baada ya kupewa wiki mbili za kuwa nje ya uwanja huku akiendelea na matibabu, haraka amerejea nyumbani kwao Zanzibar kukaa pamoja na familia yake.

“Nimepewa mapumziko na nitakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili baada ya kupata maumivu ya goti.

“Niwaondoe hofu mashabiki wa Yanga kwa kuwaambia kuwa hivi sasa Yanga ina kikosi kipana cha wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa, na huo siyo mchezo wangu wa kwanza kukosekana katika ligi.

“Ipo baadhi nilikosekana na timu ikacheza soka safi na kupata matokeo mazuri ya ushindi. Lakini nitakuwepo mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba,” alisema Fei Toto.

SOMA NA HII  HAJI MANARA AKARIBISHWA NA WAZEE WA YANGA, ATAJA DENI KWA YANGA