Home Simba SC NYOTA HAWA WAWILI WALIOMALIZANA NA SIMBA KUTANGAZWA MUDA WOWOTE

NYOTA HAWA WAWILI WALIOMALIZANA NA SIMBA KUTANGAZWA MUDA WOWOTE


 WAKATI Klabu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ikitarajia kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya kambi kuna maingizo ya wachezaji wapya wawili ambao bado hawajatambulishwa.

Ni Kibu Denis ambaye ni mshambuliaji kutoka Mbeya City, Israel Mwenda kutoka Klabu ya KMC. Wawili wametambulishwa tayari ndani ya Simba.

Nyota hao wawili wanasubiriwa kutangazwa muda wowote kwa mashabiki kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu wa 2021/22.

Winga Peter Banda yeye ameweka wazi kwamba yupo ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya kufanya kazi na anaamini kwamba kila kitu kitakwenda sawa.

Mwingine ni Yusuph Mhilu ambaye ni ingizo jipya kutoka Kagera Sugar yeye tayari ameshatambulishwa.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA KUTUA JKT...DILUNGA AFUNGUKA MAPYA KUHUSU ISHU YAKE NA SIMBA...