Home Habari za michezo HUU HAPA UKWELI WA SABABU YA NTIBAZONKIZA KUCHELEWA KUINGIA UWANJANI NA WENZAKE…

HUU HAPA UKWELI WA SABABU YA NTIBAZONKIZA KUCHELEWA KUINGIA UWANJANI NA WENZAKE…


MSHAMBULIAJI Saido Ntibazonkiza wa Yanga hakuwepo kabisa katika mstari wa wachezaji wenzake wakati wanasalimiana kabla ya mchezo dhidi ya Simba kuanza.

Wakati wachezaji wote wanaingia uwanjani na kwenda kujipanga ili mpira uanze, Ntibazonkiza yeye alichelewa kabisa kuingia uwanjani na walipokuwa wanasalimiana yeye alitoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kwenda kwenye benchi la Yanga.

Wenzake waliposalimiana na kwenda kujipanga kwa ajili ya picha ya pamoja mchezaji huyo bado alikuwa pembeni kwenye benchi.

Mpira ulipowekwa kati Ntibazonkiza aliingia ndani haraka na kwenda kucheza sambamba na wenzake akitokea upande wa kushoto.

Ntibazonkiza alipoingia uwanjani hakuonyesha kuwa na majeraha ambayo yalimfanya akose kusalimiana na wenzake pamoja na picha ya ukumbusho.

SOMA NA HII  DILI LA MWENDA KUJIUNGA SIMBA LAFIA NJIANI....ARUDI KWAKO KENYA KIMYA KIMYA...MABOSI WAGAWANYIKA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here