Home Habari za michezo KISA ARTETA…LACAZETTE NAYE KANYOOSHA MIKONO JUU ARSENAL…’AJIFUNGULIA’ MLANGO….

KISA ARTETA…LACAZETTE NAYE KANYOOSHA MIKONO JUU ARSENAL…’AJIFUNGULIA’ MLANGO….


Straika wa Arsenal, Alexandre Lacazette amefunguka na kusema kwa sasa yupo kwenye mazungumzo kwa ajili ya kuachana na timu hiyo yenye maskani yake Emirates.

Staa huyo Mfaransa mkataba wake kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Mhispaniola Mikel Arteta utafika tamati mwishoni mwa msimu huu.

Mchezaji mwenyewe, akiwa na umri wa miaka 30 kwa sasa alisema kwamba yupo kwenye mazungumzo na klabu kibao, akionyesha wazi suala la kuachana na Arsenal halina mjadala.

Akizungumza na Canal Plus, Lacazette alisema: “Nipo kwenye mazungumzo na klabu nyingi sana. Nimefungua milango.”

Fowadi huyo veterani amekuwa akihusishwa na mpango wa kurudi kwenye Ligue 1, Lyon ikidaiwa kutaka kumrejesha kwenye kikosi chao na mwenyewe amedai amekuwa akizungumza mara kwa mara na mabosi wa miamba hiyo ya Groupama.

“Sijawahi kuacha kuwasiliana na Lyon tangu nilipoondoka. Nimekuwa nikienda kwenye klabu hiyo mara moja au mbili kwa mwaka kwenda kuonana na madaktari wa timu kwa sababu ni watu wangu wa karibu. Lyon wanafahamu nipo huru, wamekuja,” alisema.

Alipoulizwa kama ana mpango wa kurudi Lyon, Lacazette alisema: “Bado kuna utata mkubwa sana. Nataka kucheza michuano ya Ulaya. Ni miaka mingi sana sijacheza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, nimemisi sana. Kuna utata, lakini kwenye maisha hakuna kisichowezekana, lakini kwa sasa bado kuna utata.”

SOMA NA HII  USAJILI WA SIMBA WASHTUA...KOCHA MPYA ASHIKILIA MAFAILI YA MASTAA HAWA