Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO….POLISI TZ WATAMBA ‘KUIPELEKEA MOTO WA KUTOSHA’ SIMBA…

KUELEKEA MECHI YA KESHO….POLISI TZ WATAMBA ‘KUIPELEKEA MOTO WA KUTOSHA’ SIMBA…


Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini amesema ubora wa kikosi chake unampa jeuri ya kuifunga Simba kesho, wakati timu hizo zitakapopambana kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza kocha huyo amesema mapumziko marefu yamewasaidia kujiandaa vizuri kwa mchezo huo, lakini pia wachezaji wake wote waliokuwa majeruhi wamepona na wapo fiti kwa ajili ya kuikabili Simba.

“Kiuhalisia mchezo utakuwa mgumu kutokana na uzoefu waliokuwa nao Simba, lakini tumejipanga vizuri kuhakikisha tunautumia vizuri uwanja wetu wa nyumbani kuifunga Simba,” amesema Malale.

Kocha huyo amesema amewaona Simba kwenye mchezo wao dhidi ya Coastal Union, ni timu ambayo ilionesha upungufu mwingi, hivyo kama watacheza kwa namna alivyowaona, basi watawafunga idadi kubwa ya mabao.

Polisi Tanzania haijawahi kuifunga Simba tangu ipande kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara, ikifungwa mechi zote za nyumbani na ugenini, kitu ambacho Malale amesema kesho wanataka kuvunja mwiko.

SOMA NA HII  ISHU YA USAJILI WA ADEBAYOR SIMBA IKO HIVI...KUMBE WAMEPIGWA DANADANA..AHMED ALL AFUNGUKA...