Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA LEO….AUSSEMS AIUA SIMBA MAPEMAA…AIBETIA YANGA USHINDI WA KISHINDO…

KUELEKEA MECHI YA LEO….AUSSEMS AIUA SIMBA MAPEMAA…AIBETIA YANGA USHINDI WA KISHINDO…


Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Aussems, raia wa Ubelgiji, ameweka wazi kuwa kwa upande wake, anaona Yanga wana nafasi kubwa katika mchezo wa leo Jumamosi dhidi ya Simba kutokana na kubebwa na rekodi ya matokeo ya mechi zao zilizopita, tofauti na wapinzani wao.

Aussems ambaye kwa sasa ni Kocha wa AFC Leopards ya Kenya, ametoa kauli hiyo kuelekea katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ambao utazikutanisha Simba na Yanga.

Aussems amesema; “Nadhani kwangu naona Yanga wanayo nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo kutokana na rekodi ya mechi za mwisho kwenye ligi, tofauti na Simba ambao wametoka kupata sare halafu wameondolewa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika. Inaonyesha kwao kukata tamaa japokuwa lolote linaweza kutokea

Patrick Aussems alifukuzwa Simba mara baada ya kushindwa kusimamia masuala ya kinidhamu kwa wachezaji pamoja na kutoifikisha timu hiyo kwenye nusu Fainal ya klabu bingwa Afrika, ambapo Simba walitolewa na TP Mazembe.

SOMA NA HII  KUPITIA SIMBA TANZANIA KUWEKA REKODI MPYA KWA MKAPA...MASHINE YA VAR KUFUNGWA...CAF WABARIKI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here