Home Habari za michezo KWA HILI SIMBA NI BABA LAO TZ….WAIKAMUA CAF ZAIDI YA BILIONI 3...

KWA HILI SIMBA NI BABA LAO TZ….WAIKAMUA CAF ZAIDI YA BILIONI 3 ‘KIUTANI UTANI TU’…BARBARA AFUNGUKA…


Simba imevuna pesa hizo zimevunwa kuanzia msimu wa 2018 kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya Simba kuifunga Nkana mabao 3-1 na kutinga hatua ya robo fainali.

Pia msimu uliofuata Simba ilishiriki tena michuano hiyo na kutinga hatua ya robo fainali kwa kumtoa As Vita mabao 4-1.

Simba kutinga hatua hizo mara mbili mfululizo ilivuna Sh 3 bilioni baada ya kupata Sh1.5 bilioni msimu wa 2018 na Sh1.5 bilioni msimu wa 2019.

Kutinga hatua hiyo sasa, Simba wanasubiri bonasi ya Sh 800 milioni kwenye mashindano hayo na kufanya kufikia Sh3.8 bilioni ndani ya miaka minne. Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alisema;

β€œKutinga hatua ya robo fainali sio mwisho wa kushiriki bado tuna kazi kubwa ya kuingia kwenye rekodi nyingine. Tunawashukuru Wachezaji kwa ujumla kwa kufikia malengo tunahamia kwenye ligi tunawekeza nguvu.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA VIDEO ZA WAZAMBIA...PABLO AGUNA KISHA AFUNGUKA HAYA...BOCCO NAYE KAMA KAWA....