Home Habari za michezo PABLO – ‘TUKIFANIKIWA HAPA…TUMEFANIKIWA PIA UGENINI’….CHAMA AONDOLEWA RASMI….

PABLO – ‘TUKIFANIKIWA HAPA…TUMEFANIKIWA PIA UGENINI’….CHAMA AONDOLEWA RASMI….


KOCHA wa Simba, Pablo Franco amesema kucheza mechi mbili ngumu ndani ya siku nne ni kati ya mambo yaliyochangia wachezaji wengi kuchoka kutokana na kutumia nguvu nyingi.

Lakini Pablo alisema anakuja na mkakati mpya na amewapa wachezaji mapumziko mafupi watarejea mazoezini kesho kujiandaa na mechi ya Jumapili dhidi ya Orlando. Kazi ya kwanza atakayoifanya ni kuwatengeneza kiakili na saikolojia ili kusahau yaliyopita na kufikiria zaidi kilichokuwa mbele yao.

“Tunamechi ngumu na Pirates kikubwa tunachohitaji kila mchezaji kufikiria zaidi mchezo huo kupambana vya kutosha ili kupata ushindi mkubwa itakaotuweka katika mazingira mazuri,” alisema Pablo na kuongeza;

“Tukifanikiwa kupata ushindi mkubwa nyumbani maana yake tunajirahisishia kazi kwenye mchezo wa marudiano ugenini Afrika Kusini kwahiyo sasa nguvu na akili zetu zinatakiwa kuwa hapa.”

KUHUSU CHAMA

Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola alisema sababu ya kumuweka nje mchezaji kama Clatous Chama dhidi ya Polisi Tanzania ni kwavile hayupo kwenye mipango ya mchezo wa Pirates.

Alisema waliamua kumuweka Chama benchi ili yule atakayeanza kwenye mechi ya robo fainali atumie mechi hiyo ya Polisi Tanzania kama mchezo wa kuandaa mwili wake na kupata muda wa kutosha.

“Ingawa kwenye kipindi cha pili tulimpa nafasi Chama ila matokeo hayakuwa bora kwa upande wetu kwani tulikuwa tunahitaji pointi tatu,”

“Sababu ya mwisho tunacheza mechi ngumu za zenye ushindani kila baada ya muda mfupi kuna wachezaji walikuwa wamechoka, wengine wanaumwa tukaamua kufanya mabadiliko hayo ya wachezaji nane kwenye kikosi cha kwanza.”

Wachezaji watatu wa kikosi cha kwanza Simba walioanza kwenye mechi hiyo iliyomalizika kwa suluhu dhidi ya Polisi Tanzania walikuwa, Shomary Kapombe, Rally Bwalya na Chriss Mugalu.

Kulingana na viwango walivyoonyesha wachezaji wa Simba nafasi ya beki wa kati kwenye mechi ya Pirates baada ya kukosekana Onyango anaweza kuanza Wawa wakati pale kwa Kanoute anaweza kuanza, Mzamiru.

Wachezaji wengine waliopata nafasi ya kucheza si wa kikosi cha kwanza walikuwa, Benno Kakolanya, Gadiel Michael, Pascal Wawa, Kennedy Juma, Erasto Nyoni, Mzamiru Yassin, Meddie Kagere na Yusuph Mhilu.

SOMA NA HII  KIGWANGALA : JEZI NZURI ILA MJADALA WA BILIONI 20 ZA MO DEWJI UKO PALE PALE....NIMEAMUA KUNYAMA NISIHARIBU LADHA...