Home Habari za michezo SAA CHACHE KABLA YA KUSHUKA UWANJANI…PABLO AIBUKA NA JIPYA SIMBA..AFUNGUKA HALI...

SAA CHACHE KABLA YA KUSHUKA UWANJANI…PABLO AIBUKA NA JIPYA SIMBA..AFUNGUKA HALI ILIVYO…


Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Franco Pablo Martin amesema wachezaji wake wamekamilisha Program ya maandalizi kabla ya kuikabili USGN leo Jumapili (April 03) saa nne usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salaam.

Kikosi cha Simba SC kilifanya mazoezi ya mwisho jana Jumamosi (April 02) Usiku, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ambako mchezo dhidi ya USGN utapigwa leo Jumapili (April 03).

Kocha Pablo amesema wachezaji wake wamepata muda mzuri wa kujiandaa na mchezo huo, na Uongozi umefanya kazi yake ipasavyo kwa kumtimizia mahitaji yote aliyoyawasilisha juma moja kabla ya kuanza kambi.

Amesema kwa misingi hiyo anaamini wachezaji wake watapambana kwa kutumia mbinu alizowafundisha karibu juma zima, hivyo amewataka mashabiki kuendelea kuwa na imani na kikosi chao kitakachoikabili USGN baadae leo Jumapili (April 03).

“Jambo jema tulikuwa na muda wa kujiandaa na mchezo, wachezaji wapo tayari kimwili na akili na wanajua umuhimu wa huu mchezo kwa maisha yao ya soka.”

“Uongozi umekamilisha kila hatua iliyotakiwa kufanywa katika maandalizi ya kikosi changu, sina shaka tutapambana na kupata matokeo chanya ambayo yatatuvusha na kutupeleka kwenye hatua nyingine ya michuano hii” amesema Kocha wa klabu ya Simba SC, Pablo

Simba SC inahitaji kushinda dhidi ya USGN ili ifikishe alama 10, zitakazoivusha kwenda Robo Fainali, huku Mshiriki mwingine kutoka Kundi D, katika hatua hiyo akitarajiwa kupatikana baada ya mchezo wa RS Berkane ya Morocco itakayokua nyumbani dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Msimamo wa Kundi D unaonyesha ASEC Mimosas inaongoza ikiwa na alama 09, ikifuatiwa na RS Berkane yenye alama 07 sawa na Simba SC, huku USGN ikiburuza mkia kwa kufikisha alama 05.

SOMA NA HII  YANGA WALAMBA SHAVU KUTOKA SHIRIKA LA BIMA LA NIC