Viongozi wa Klabu ya Al Ahly, jana walikaa kikao na Benchi la Ufundi la Klabu hiyo pamoja na Wachezaji wote kujadili juu ya Mwenendo wa Klabu hiyo Baada ya Jana kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Ceramica Cleopatra kwenye Mchezo wa Ligi Kuu Misri (Egypt Premier League).
Mpaka sasa Al Ahly wamecheza michezo 14 ya Ligi Kuu Misri na kufanikiwa kukusanya alama 33 wakishika nafasi ya pili nyuma ya Vinara Zamalek mwenye pointi 38 lakini anamzidi Al Ahly Michezo Miwili.
Licha ya Mafanikio waliyoyapata Al Ahly chini ya Kocha Pitso Motsmane lakini baadhi ya viongozi na Mashabiki wa Klabu hiyo wanataka Kocha huyo afukuzwe.
Miongoni mwa mafaniko makubwa waliyoyapata Al Ahly chini ya Kocha Mkuu Msauzi Afrika Pitso Motsmane ni pamoja na kutwaa Ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka jana na mwaka juzi, kufika hatua ya Nusu Fainal ya Kombe la Klabu Bingwa ya dunia mwaka huu, pamoja na kuifanikisha timu hiyo bora ya karne ya CAF kufika tena Nusu fainali ya Klabu Bingwa Afrika Msimu huu.