Habari za michezo

AHMED ALLY : NISIWE MNAFIKI…TUNAWAOMBEA YANGA MABAYA …ADUI MUOMBEE NJAA….

admin May 12, 2022 10:19 am


Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema wanaiombea mabaya Young Africans ili ipoteze michezo inayowakabili kabla ya msimu huu kufikia ukingoni.

Ahmed ametoa kauli hiyo baada ya Simba SC kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Kagera Sugar jana Jumatano (Mei 11), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Ahmed amesema: Pasina kuwa mnafiki niseme kwamba tunawaombea mabaya, alisema Afande Sele ‘Adui muombee njaa.”

Katika hatua nyingine Ahmed amesema baada ya kumalizana na Kagera Sugar, kikosi cha Simba SC kimeanza maandalizi ya mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Pamba FC, utakaopigwa Jumamosi (Mei 14) Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Tumemnyoa Kagera Sugar hapa Dar es salaam, tunamsubiri Pamba FC katika mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ naye tuje tumalizane naye, tuelekee hatua inayofuata. amesema Ahmed Ally

Mchezo huo ulipaswa kuchezwa mwezi April, lakini uliahirishwa kufutia Simba SC ilikua inakabiliwa na mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

KUELEKEA MSIMU UJAO…GEORGE MPOLE ATOA SHARTI HILI TU ASAINI YANGA CHAP….AITAJA NAFASI YA MAYELE…. BAADA YA KUICHAPA KAGERA JANA…KAPOMBE AVUNJA UKIMYA SIMBA…AFUNGUKA WALICHOKUBALIANA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply