Home Habari za michezo KUELEKEA MSIMU UJAO…GEORGE MPOLE ATOA SHARTI HILI TU ASAINI YANGA CHAP….AITAJA NAFASI...

KUELEKEA MSIMU UJAO…GEORGE MPOLE ATOA SHARTI HILI TU ASAINI YANGA CHAP….AITAJA NAFASI YA MAYELE….


Ikiwa ni baada ya tetesi nyingi kuzagaa kuhusishwa kusaini mkataba Yanga, mshambuliaji wa Geita Gold, George Mpole ametoa sharti moja kubwa kwa timu hiyo.

Mpole ni kati ya wachezaji wanaohusishwa kutua Yanga kuelekea msimu ujao ambapo timu hiyo ina uhakika wa kushiriki michuano ya kimataifa inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Mshambuliaji huyo hivi sasa yupo katika vita kubwa ya kuwania ufungaji bora ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu akifukuzana na straika wa Yanga, Mkongomani, Fiston Mayele. Kabla ya jana, wote walikuwa na mabao 12.

Mpole alisema timu zote zinazomuhitaji kwa ajili ya kuzungumza naye ili kumsajili, hivi sasa zimuache kwanza atimize majukumu yake katika kikosi cha Geita Gold.

Mpole alisema, hivi sasa akili yake ameiweka ndani ya Geita Gold kwa ajili ya kuipambania imalize ligi katika nafasi nzuri katika msimamo ambapo wanashika nafasi ya nne wakikusanya pointi 31.

“Zipo taarifa nyingi kunihusisha kuhitajika na baadhi ya timu za ligi kuu hapa nyumbani, lakini huu sio muda muafaka kwangu kuanza kufanya mazungumzo na timu yoyote.

“Kikubwa sitaki kuvuruga akili yangu, hivi sasa nguvu zangu nimezielekeza katika kuipambania timu yangu kwa michezo iliyobaki, lengo likiwa ni kumaliza tukiwa katika nafasi nne za juu.

“Hivyo hizo timu zinazonihitaji naomba ziniache kwanza hadi pale ligi itakapomalizika ndiyo tuanze kukaa meza moja kwa ajili ya kufanya mazungumzo.

“Hadi hivi sasa bado sijaamua hatma yangu wapi ninakwenda msimu ujao, nitatoa kipaumbele kwa timu yangu ya Geita Gold kabla ya kuchukua maamuzi mengine,” alisema Mpole.

MAYELE AMPA JEURI

Akizungumzia kasi yake ya ufungaji mabao katika Ligi Kuu Bara msimu huu, Mpole amesema siri iliyopo nyuma ya uwezo wake huo ni ushindani dhidi ya wachezaji wengine akiwemo Mayele.

“Nafikiri ligi yetu kwa sasa imekuwa sana na inatazamwa na nchi nyingi za Afrika, hivyo kwangu na wachezaji wazawa tunaitumia hiyo kama nafasi ya kufanya vizuri zaidi ili tuonekane.

SOMA NA HII  WAKATI HATA UHAKIKA WA KUPATA NAFASI HAUPO...NKANE AIBUKA NA HAYA MAPYA KWA YANGA...'AJIPALILIA MOTO JIKONI'...

“Lakini pia hawa wachezaji wakigeni tunaocheza nao, wamekuwa na mchango mwingine kwetu kwani tumekuwa tukiwatazama wanavyocheza na kufunga ili nasi tuwe bora kama wao viwanjani,” alisema.