KUFUATIA taarifa ya kupewa mapumziko mpaka mwishoni mwa msimu huu, kiungo mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, ameibua mapya kikosini hapo.
Morrison ambaye mkataba wake na Simba unamalizika mwisho wa msimu huu, alijiunga na timu hiyo msimu wa 2020/21 baada ya kuondoka Yanga.
Juzi Ijumaa baada ya kupewa likizo hiyo, aliwaaga wenzake kambini huku akiwataka kuhakikisha wanapambana kufikia malengo waliyojiwekea msimu huu.
Morrison alisema: โNiko hapa kwa dhumuni moja kubwa la kurejesha shukrani zangu za dhati kwenu nyote katika kipindi ambacho nimekuwa mchezaji wa Simba.
โLicha ya kwamba mimi bado ni mchezaji wa Simba kimkataba, lakini kwa manufaa mapana ya klabu hii na mimi binafsi, sitaendelea kuwa na timu mpaka mwishoni mwa msimu.
โSina tatizo lolote na uongozi na nawatakia kila la kheri mpaka pale tutakapokutana tena.โ
Morrison wakati anaondoka kambini, alionekana akiwa ameshika blanketi lake na mabegi ikionesha kwamba amebeba kila kilicho chake, huku kiungo wa timu hiyo, Mzamiru Yassin akimtania kuwa anaenda Yanga.