Habari za michezo

BAADA YA MWAMNYETO KUONGEZA MKATABA MPYA YANGA…WAKALA WAKE AIBUKA NA HILI…ATAJA MKATABA ULIOPITA…

admin May 18, 2022 2:51 am


BEKI na Nahodha wa Yanga Bakari Mwamnyeto ataendelea kubaki ndani ya klabu hiyo kwa miaka mingine miwili.

Mwamnyeto amesaini dili hilo leo jioni mbele ya wafadhili wa Yanga GSM mkataba huo ambao sasa utamfanya kuitumikia klabu hiyo kwa jumla ya miaka minne.

Meneja wa beki huyo wa zamani wa Coastal Union Kassa Mussa amezungumza akiwa Italia akithibibitisha hatua hiyo.

“Tumeamua kubaki Yanga kwa kuwa ni klabu ambayo tumekubaliana na kijana wangu (Mwamnyeto) kubaki baada ya kuona mafanikio mazuri katika mkataba wa kwanza” amesema Kasa.

Tangu atue  Yanga Mwanyeto amekuwa na mafanikio makubwa ndani ya klabu hiyo akijihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza huku pia akipewa unahodha ndani ya klabu hiyo kongwe.

Hatua hiyo inaifanya Yanga kushinda vita muhimu kufuatia watani wao Simba na Azam kuwa katika mbio za kuwania saini ya beki huyo wa zamani wa Coastal Union.

INJINIA HERSI :- MORRISON NI BONGE LA WINGA….AJE KWETU YANGA APUMZIKE …HATUNA SHIDA SIE… MCHAGA WA KILUVYA ALIYESHINDA JACKPOT YA SportPesa.. AKABIDHIWA UBILIONEA WAKE LEO….AFUNGUKA ALICHOFANYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply