Home Habari za michezo KUELEKEA MSIMU UJAO…YANGA KUPIGA CHINI MASTAA HAWA 6…KUSHUSHA VIFAA VIPYA VINNE…MORRISON NA...

KUELEKEA MSIMU UJAO…YANGA KUPIGA CHINI MASTAA HAWA 6…KUSHUSHA VIFAA VIPYA VINNE…MORRISON NA PHIRI NDANI…..


YANGA inaamini ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu na baada ya kutimiza hilo, wamepanga kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo watashiriki msimu ujao.

Kwa kutambua hilo, uongozi wa timu hiyo kwa kushirikiana na wadhamini wao GSM wamepanga kufanya usajili wa gharama kubwa ambao utaifanya kutimiza lengo hilo lakini pia kutikisa katika Ligi ya Mabingwa.

Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezinasa ni kuwa Yanga imetenga kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya usajili wa nyota wapya ambao inaamini wataongeza nguvu katika kikosi chao.

Pamoja na ubora na mafanikio ya kikosi chake msimu huu, Yanmga inaamini kwamba yapo maeneo ambayo yanapaswa kuimarishwa zaidi kwa kuleta wachezaji wapya ambao ama wataingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza au kuleta ushindani kwa wale wanaoanza ili kutoa wigo mpana kwa benchi lake la ufundi katika uteuzi wa kikosi.

Ili kupisha ujio wa wachezaji hao wapya, Yanga imepanga kuwatoa kwa mkopo baadhi ya wachezaji na wengine kuwapa mkono wa kwaheri moja kwa moja.

WAGENI WANNE

Yanga inaamini kwamba kikosi ilichonacho ili kitambe kimataifa na kufika katika hatua za juu za Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, inapaswa kuongeza takribani nyota wanne wa kigeni wa daraja la juu ambao wana uzoefu wa mashindano ya kimataifa.

Usajili wa nyota hao wanne pekee, utaifanya Yanga kutumia zaidi ya Sh 800 milioni ambazo zitatumika kama dau la usajili na gharama za kuvunja mikataba kwa wale ambao bado hawajamaliza.

Wageni hao wanne ambao watasajiliwa, ni winga mmoja, mshambuliaji mmoja wa kati, kiungo mshambuliaji, kiungo mkabaji pamoja na beki wa kushoto.

Yanga inataka kuleta kiungo mshambuliaji ambaye ana uwezo mkubwa wa kupiga pasi za mwisho na katika orodha yao miongoni mwa majina ni nyota wa Asec Mimosas, Aziz Ki(anayewindwa pia na Zamalek ya Misri) lakini upande wa winga, jina la mchezaji wao wa zamani aliyetemwa na Simba, Bernard Morrison limewekwa katika hesabu zao. Wengine ambao wanatajwa kuwaniwa ni washambuliaji Victorien Adebayor na Moses Phiri pamoja na beki Mustafa Kiiza.

USAJILI KIMKAKATI

Uamuzi wa kumsajili kiungo mkabaji wa kimataifa unalenga kumrudisha nyuma Yannick Bangala kucheza kama mlinzi wa kati kwa kile ambacho klabu hiyo inahofia kuwa kimo cha beki wake Dickson Job anayecheza sambamba na Bakari Mwamnyeto kinaweza kuwagharimu katika mechi za kimataifa.

Yanga imepanga kumnasa kiungo mahiri mwenye uwezo wa kuilinda safu ya ulinzi, kupiga pasi na kuisogeza timu mbele ambaye atakuwa akipangwa sambamba na Khalid Aucho na kisha Bangala kucheza kama mlinzi wa kati nafasi ambayo anaimudu vyema.

SOMA NA HII  KUMBE! WADUKUZI WALIHACK NAMBA YA MWENYEKITI WA YANGA

“Changamoto kubwa ya Dickson Job ni kimo chake. Ni mchezaji mzuri na ana uwezo mkubwa lakini mechi za Ligi ya Mabingwa ni tofauti na mashindano ya ndani. Kule timu nyingi zina washambuliaji warefu ambao ukifanya kosa ni rahisi kukuadhibu,” kilisema chanzo cha uhakika ndani ya klabu hiyo.

Lakini pia Yanga imeona inahitajika kusajili beki wa kimataifa wa kushoto kwani waliopo wanaonekana kushindwa kumudu vyema majukumu jambo lililopelekea kutumika kwa wachezaji wawili ambao kiasili hawacheza nafasi hiyo ambao ni Shomary Kibwana na Farid Musa.

PANGA LANYEMELEA SITA

Wachezaji takribani sita watapewa mkono wa kwaheri kwa kuvunjiwa mikataba yao au kutoongezwa mipya baada ya ile ya awali kumalizika kutokana na viwango vyao kutoridhisha na kutoonekana kama wanaweza kuwa na mchango mkubwa.

Makipa Erick Johora na Ramadhan Kabwili watatupiwa virago moja kwa moja sambamba na Deus Kaseke, Chico Ushindi, Heritier Makambo na Paul Godfrey ‘Boxer’.

Johora, Kabwili, Makambo na Ushindi mikataba yao itavunjwa wakati Kaseke na Boxer hawataongezewa mipya.

WANNE MKOPO

Mshambuliaji wa Burkina Faso, Sogne Yacouba ataongezwa mkataba, lakini atatolewa kwa mkopo ili apate timu itakayompa nafasi ya kutosha ya kucheza aweze kurudisha ufiti kama ilivyothibitishwa na Mjumbe wa Kamati ya Mashindano, Injinia Hersi Said. “Tulimsainisha (mkataba) akiwa bora na mzima kaipambania timu akaumia akiwa kwenye majukumu yake ndani ya Yanga. Tumepambana kumtibia kwa kila hali sasa anachosubiri ni ruhusa ya kucheza kwanini tumtelekeze?

“Tuna mpango wa kuendelea kubaki naye lakini ili kuhakikisha anakuwa fiti tutamtoa kwa mkopo kwenda timu ambayo itampa nafasi ya kucheza mara kwa mara ili kurudisha ubora na akiwa fiti tutamr udisha,î alisema Hersi.

Nyota wengine ambao Yanga huenda ikawatoa kwa mkopo ni beki David Bryson, winga Ducapel Moloko na mshambuliaji Yusuph Athuman.

MASTAA KIKAANGONI

Ujio wa nyota wapya huenda ukawafanya baadhi ya nyota wanaotamba katika kikosi cha Yanga sasa kupoteza nafasi katika kikosi cha kwanza iwapo watashindwa kukaza buti.

Mbali na Job ambaye anaweza kuwa na kibarua kigumu kutokana na Bangala kurudishwa kucheza nafasi ya beki wa kati, mwingine ambaye anapaswa kupambana ni Kibwana Shomary ambaye kwa sasa anatumika kama beki wa kushoto huku kulia akiwepo Djuma Shaban.

Feisal Salum na Saido Ntibazonkiza ambao wanacheza nafasi ya kiungo mhambuliaji, wanaweza kujikuta nao waisotea benchi kupisha ingizo la nyota mpya atakeysajiliwa katika nafasi ya kiungo msh ambuliaji.