Simba SC

KISA SIMBA SC, AL-MERRIKH YA SUDAN WAMFUKUZA KAZI KOCHA WAO MPYA

admin February 3, 2021 5:32 pm


KATIKA kinachoonekana bado suala la Simba kuwapora kocha wao, Didier Gomez De Rosa, limewapa mchecheto, Al-Merrikh kumtimua kocha wao Miodrag Jesic, raia wa Serbia, siku saba tu tangu ilipomtambulisha rasmi.

Januari 25, mwaka huu, Al-Merrikh ilimtangaza Jesic kumrithi De Rosa aliyetimkia Simba, lakini jana klabu hiyo ya Sudan iliyopangwa na Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika iliachana naye pasipo kutaja sababu.

β€œAl-Merrikh inatangaza kuvunja mkataba na Mserbia Miodrag Jesic na kumtangaza Mbelgiji mwenye asili ya Tunisia, Nasreddine Nabi kama kocha mkuu. Nabi ni kocha wa zamani wa Ahli Benghazi ya Libya, Al Hilal ya Sudan na Ismaily ya Misri, atawasili jioni hii (jana) kuanza safari yake na sisi,” ilisema taarifa ya klabu hiyo.

Al-Merrikh imepangwa kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika na Simba, Al Ahly na AS Vita Club ambapo timu mbili zitakazoongoza kila kundi zitafuzu robo fainali.

YANGA WAFUNGUKIA ISHU YA USAJILI WA LUIS ANAYECHEZA SIMBA MORRISON:- SIWANASEMA NINA ‘BUSHA’…? WAJIANDAE KUKEREKA ZAIDI..!!

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply