Habari za michezo

IBENGE AWANIA UKOCHA MALI, AZAM FC YATAZAMA MUSTAKABALI WAKE

Vardo May 20, 2026 9:25 am

KOCHA mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge, ameibuka miongoni mwa majina matano yaliyoingia hatua ya mwisho katika mchakato wa kuwania nafasi ya ukocha mkuu wa timu ya taifa ya Mali, hatua inayoonesha jinsi anavyoendelea kuvutia katika soka la Afrika.

Ibenge, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa sasa anaendelea na majukumu yake ndani ya Azam FC ambapo mkataba wake unatarajiwa kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu, hali inayofanya mustakabali wake kuwa gumzo.

Shirikisho la Soka la Mali (Mali FA) lilipokea jumla ya maombi 28 kutoka kwa makocha mbalimbali duniani waliotaka kuinoa timu hiyo ya taifa, kabla ya kufanya mchujo mkali uliobaki na wagombea watano pekee.

Katika orodha hiyo ya mwisho, wapo makocha wawili kutoka Ureno, mmoja kutoka Morocco, mmoja kutoka Mali mwenyewe, pamoja na Ibenge kama mwakilishi pekee kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Taarifa zinaeleza kuwa bodi ya uteuzi ya Mali FA kwa sasa ipo katika hatua za mwisho za tathmini ya kila mgombea, ikizingatia uzoefu, mafanikio na uwezo wa kiufundi kabla ya kutoa uamuzi rasmi.
Uamuzi wa mwisho kuhusu nani ataichukua mikoba ya kuinoa Mali unatarajiwa kutangazwa hivi karibuni.

SIMBA YATAWALA ARUSHA, REKODI NZURI YAZUA HOFU KWA COASTAL UNION TETEMEKO LAANZA TANZANIA CHAMA AMGEUZIA SIMBA NGUVU MPYA