Habari za michezo

KUELEKEA MSIMU UJAO…DEO KANDA AFUNGUKA ISHU YA KURUDI TENA SIMBA….AITAJA YANGA….

admin May 21, 2022 2:30 pm


Mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Simba, ambaye kwa sasa anaitumikia Mtibwa Sugar, Deo Kanda amesema malengo yake ni kuhakikisha anarejea katika vilabu vikubwa vya soka hapa nchini Tanzania.

Kanda ambaye ni raia wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, amesema yupo Mtibwa ili kupata muda mwingi wa kucheza utakaomuwezesha kurejea katika vilabu vikubwa japo hakuvitaja.

Nyota huyo aliyejiunga na Simba kwa mkopo akitokea TP Mazembe, amesema Tanzania ni sehemu sahihi kwake kucheza soka na kuna ushindani mkubwa jambo ambalo ana amini ndilo linawafanya wachezaji kutoka Congo kuamua kuja kucheza Ligi Kuu Tanzania bara.

”Nipo Mtibwa ili nipate muda wa kucheza mara kwa mara, ninahitaji kurejea kwenye vilabu vikubwa Tanzania”alisema Deo Kanda.

Katika hatua nyingine Kanda ameipa Klabu ya Yanga nafasi kubwa ya kuwa bingwa msimu huu kutokana na kujiimarisha zaidi ya timu nyingine.

”Ligi ni ngumu msimu huu,lakini kwa mwenendo ulivyo hata kama mechi za kucheza bado nyingi lakini ninaona Yanga itachukua ubingwa ”Deo Kanda.

Kuhusu kurejea Simba, Deo Kanda amesema yupo tayari kwa kuwa ni timu aliyoitumikia hivyo iwapo watahitaji huduma yake hatosita kuwatumikia.

TETESI ZA USAJILI ULAYA…WAKALA ASHINIKIZA LEWANDOWSKI KUTUA BARCELONA…ANUNUA JEZI KUMI ZA BARCA…. IBENGE NA RS BERKANE WAFANYA KWELI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA….WABEBA NDOO KIBABE MBELE YA WASAUZI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply